Search This Blog
Saturday, November 16, 2019
Mtoto wa Miezi Mitano Atelekezwa Nyumba ya Kulala Wageni Njombe
Na Amiri kilagalila-Njombe
Jeshi la polisi mkoa wa Njombe limefanikiwa kumpata mtoto wa miezi mitano aliyetelekezwa nyumba ya kulala wageni na kumuhifadhi chini ya uangalizi wa idara ya ustawi wa jamii.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Njombe Hamis Issa ametoa taarifa hiyo kwa wanahabari mkoani humo akibainisha kuwa mtoto huyo amekutwa kwenye nyumba ya kulala wageni inayofahamika kama Shamba Guest House iliyopo mjini Njombe huku akiacha ujumbe wa kuelekea mwanza .
“Shamba Guest amekutwa mtoto ambaye ana umri mdogo zaidi na ametelekezwa na mwanamke ambaye ni mama yake na ameacha ujumbe amesema anaenda eneo la Mwanza na huyu msaidizi amemuachia huyo mtoto,na pindi mambo yatakapo kuwa mazuru atamtumia hela”anasema Hamis Issa
Kwa mujibu wa kamanda mwanamke huyo anafahamika kwa jina la Stella Mtweve na mtoto huyo wa kiume mwenye umri wa miezi mitano na nusu ametambuliwa kwa jina la Kelvin Mmagoma
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment