Waziri Mku wa Uingereza Boris Johnson siku ya Jumatatu atazungumza na viongozi wa Ujerumani, Ufaransa na rais wa Halmashauri ya Umoja wa Ulaya katika jaribio la kuwataka viongozi hao waunge mkono mkataba wake Brexit.
Hayo yameelezwa na gazeti la Times la nchini Uingereza likinukuu chanzo kinachofahamu mipango ya mazungumzo hayo.
Wakati wa mazungumzo hayo na Kansela Angela Merkel, rais Emanuel Macron na Jean Claude Junker, Johnson atawarai viongozi hao wamsaidie kupata mkataba wa Brexit wiki inayokuja au waridhie Uingereza ijitoe kutoka Umoja wa Ulaya bila makubaliano ifikapo Oktoba 31.
Wajumbe wa mazungumzo ya Brexit kutoka Uingereza na Umoja wa Ulaya, waliingia kwenye mazungumzo magumu ya mwishoni mwa juma kutafuta njia ya kuondoa mkwamo wa Brexit kuelekea mkutano wa kilele wa Umoja wa Ulaya baadae wiki ijayo.
Search This Blog
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment