Search This Blog

Wednesday, October 16, 2019

Wapongeza kituo cha msaada wa kisheria


 Na Ahmad Mmow- Mbinga

Halmashauri ya wilaya ya Mbinga vijijini imekipongeza  kituo cha msaada wa kisheria cha NAJATA kilichopo katika mji wa Mbinga kwa juhudi kubwa ya kusuluhisha na kutatua migogoro ya kijamii katika halmashauri hiyo.

Pongezi hizo zimetolewa leo mjini Mbinga na kaimu mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo, Paschal Ndunguru alipozungumza na Muungwana Blog mjini Mbinga.

Nduguru alisema kituo hicho ni msaada katika kusuluhisha na kutatua migogo katika jamii ndani ya halmashauri hiyo. Kitendo ambacho ni msaada mkubwa kwa halmashauri hiyo kupitia idara ya maendeleo ya jamii.

Nduguru ambae ni mkuu wa idara ya maendeleo ya jamii wa halmashauri hiyo alisema kuna ushirikiano mkubwa baina ya kituo hicho na halmashauri hasa katika utoaji elimu kuhusu ukatili wa kijinsia, mimba za utotoni, mirathi, matunzo ya watoto na utatuzi wa migoro ya ardhi na ndoa.

''NAJATA ndio waliofanya ushawishi hadi kufanikisha kikundi cha watu wenye ulemavu kupata fedha takribani shilingi milioni 40 kutoka kwa mhisani,''  alisema Ndunguru.

Mkuu huyo wa idara ya maendeleo ya jamii alikiri kwamba kuna unyanyasaji wa kijinsia ambao unatazamwa na kuchukuliwa kama jambo la kawaida na sehemu ya utamaduni.

 ''Wanaume wanajiona wana haki zaidi katika umiliki wa mali. Hata hivyo kadiri elimu inavyoendelea kutolewa vitendo hivyo vinapungua. Lakini siyo jambo linaloweza kuondoka ghafla na haraka maana tabia hiyo ni kama utamaduni wa maeneo haya,'' alisema Ndunguru.

Aidha Nduguru alisema halmashauri hiyo ipo kwenye mkakati kabambe wa kuendelea kutoa elimu kuhusu mambo hayo ambapo sasa wamewashirikisha waratibu wa elimu wa kata wasaidie kutoa elimu kupitia elimu ya watu wazima.

Aliweka wazi kwamba NAJATA kwa upande wake inasaidia sana sekta ya elimu kwa kushiriki kikamilifu mapambano dhidi ya ndoa na mimba za utotoni na utoro shuleni.

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...