Search This Blog
Saturday, October 26, 2019
Wanachi watakiwa kutumia vyema wiki ya sheria
Na. Rahel Nyabali, Tabora
Kufuatiwa wiki ya sheria nchini wananchi mkoani tabora wametakiwa kutumia wiki hiyo vyema ili kuweza kupata msaada wa kisheria hasa wasio na uwezo kujua matatizo yanayowakabili yanayohitaji msaada wa kisheria kwakuwa wengi wao wamekuwa wakijikuta wanapoteza haki zao kutokana na kutojua sheria hasa wanapokuwa wakikabiliwa na mashauri mbalimbali mahakamani.
Hayo yameelezwa katika mdahalo ulio hudhuliwa na wadau mbalimbali mkoani humo wakati ambapo Chama cha Wanasheria TLS kanda ya Tabora kikiwa katika wiki ya msaada wa kisheria kimeadhimidhimisha wiki hiyo kwa kufanya mijadala juu ya umuhimu wa Sheria ya msaada wa kisheria ambapo kimsingi wananchi hasa wanyonge wanapaswa kufaidika nayo.
Charles ayo ni mmoja wa Wakili wa Kujitegemea mkoani Tabora amesema kufuati wiki hii ya sheria ambapo wameweza kukutana baadhi ya wananchi na wadau wa masuala ya kisheria katika mjadala unaohusu Sheria ya msaada wa kisheria na umuhimu wake hasa kwa wananchi wenye mahitaji na wasio na uwezo kutaweza kusaidia kwa kiasi kikubwa kupata uelewa kwa wananchi na kujua haki zao.
Mkazi wa Tabora Sophia martin ni moja ya mwananchi aliye pata wasaa wa kuchangia kwenye mdahalo huo amesema watu wengi hasa wa kijijini kwa kiasi kikubwa hawana elimu juu ya huduma ya sheria hivyo amewaomba wanasheria kuwafikia watu hao ili kupata haki zao.
Hata hivyo katika kuadhimisha wiki ya msaada wa kisheria Chama cha Wanasheria TLS Kanda ya Tabora wmeweza kufika katika magereza ya Urambo,Nzega na Gereza kuu la Uyui ili kubaini mahitaji ya msaada wa kisheria kwa watu waliopo Magerezani.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano anayeshughulikia Sekta ya Ujenzi, Arch. Elius Mwakalinga, akitoa maelekezo kwa Kai...


No comments:
Post a Comment