Search This Blog
Monday, October 7, 2019
Waajiri chanzo cha migogoro ya wafanyakazi - Dkt. Mary Mwanjelwa
Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Manejimenti ya Utumishi, Umma na Utawala Bora, Dk. Mary Mwanjelwa amesema waajiri wengi nchini wamekuwa hawatimizi majukumu yao ipasavyo hali inayosababisha uwepo wa migogoro sehemu zao za kazi.
Dkt. Mwanjelwa ameyasema hayo wakati akizungumza na baadhi ya watumishi wa umma katika kikao kazi kilichofanyika kwenye ukumbi wa Shule ya Msingi Bariadi Allience Mjini Bariadi.
"Sisi viongozi tuliopewa mamlaka husika ya kusimamia sekta ya utumishi wa umma ni lazima tusimamie sheria na taratibu zinazotakiwa hivyo basi serikali ya awamu ya tano kamwe haitaweza kulifumbia macho suala la waajiri hao kuwaonea na kuwanyanyasa waajiriwa wao,” amesema Dk Mwanjelwa.
Amesema kuwa waajiri wengi wamekuwa wakijiona wao kuwa ni Mungu watu hivyo hata utendaji wao wa kazi umekuwa haufuati taratibu na kanuni za utumishi wa umma na kwamba mara nyingi wamekuwa wakifanya kazi kwa mazoea na kusababisha uminyaji wa uhuru na haki za watumishi wa umma.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment