Search This Blog

Monday, October 7, 2019

Rais Magufuli awacharukia wanaowapa mimba wanafunzi


Rais wa Tanzania, Dkt. Pombe Magufuli amewataka wakazi wa Mkoa wa Rukwa kuacha tabia ya kuwapa ujauzito wanafunzi na badala yake kutafuta watu ambao wameshamaliza shule.

Ametoa kauli hiyo, alipokuwa akizungumza na wananchi katika uwanja wa Mandela baada ya kuzindua mradi wa maji safi na mazingira na Msikiti wa Istiqaama uliopo eneo la Majengo mkoani humo.

“Kwa takwimu nilizo nazo Mkoa wa Rukwa ni miongo mwa mikoa inayowapa wanafunzi ujauzito, nimeambiwa kwa mwaka jana tu wanafunzi 229 walipata ujauzito, tumeeleza tumekua ukitoa fedha kwaajili ya elimu bure kwa watoto wetu ninyi mnatoa mimba bure sasa tutakuwa tunatoa hela kumbe tunapata hasara,”

“Ninajua mnakula vyakula vyenye nguvu mkatafute ambao wamemaliza muda wao, msiwaonee hawa wanafunzi na nyie watoto muache viherehere mtayakuta tu baadae kwahiyo hili ni lazima tulisimamie na nyie wazazi tuwafundishe watoto wetu yani unamuona kila siku anaenda kusoma hata daftari hana na unamuacha tu,”

“Hawa ni watoto masikini tusiwarubuni kwakuwa ni malaika na vyombo vya dola muanze kuwashughulikia hawa watu wanaowapa mimba kwani sheria inajulikana ni miaka 30 akishaenda gerezani ataelewa nini maana ya mimba, hii ni aibu kubwa katika mkoa wenu,” alisema.




No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...