Search This Blog
Sunday, October 13, 2019
Uniti 10 za damu salama zakusanywa kwenye mkesha wa Mwenge wa Uhuru Kilwa
Na Ahmad Mmow, Lindi.
Jumla ya uniti kumi za damu salama zimekusanywa katika mkesha wa Mwenge wa Uhuru katika viwanja vya bustani ya Mkapa( Mkapa garden) halmashauri ya mamlaka ya mji mdogo wa Kilwa Masoko.
Hayo yameelezwa leo na mkuu wa wilaya ya Kilwa, Christopher Ngubiagai wakati anakabidhi Mwenge wa Uhuru kwa halmashauri ya manispaa ya Lindi, mtaa wa Mtomkavu.
Ngubiagai alisema katika mkesha huo kulikuwa na uchangiaji damu salama, wananchi waliojitokeza kuchangia walifanikiwa kutoa uniti kumi za damu salama.
Mbali ya damu salama, lakini pia mkuu huyo wa wilaya ya Kilwa alisema watu 47 walijitokeza kupimwa ili kuona kama wanavimelea vya ugonjwa wa malaria. Katika zoezi hilo ni watu wanne tu waliobainika kuwa na vimelea vya ugonjwa huo.
Lakini pia watu 247 walijitokeza kupima maambukizi ya Virusi Vya UKIMWI( VVU). Katika upimaji huo wa maambukizi ya VVU ni mtu mmoja tu alikutwa na maambukizi,'' alisema Ngubiagai.
Katika halmashauri ya wilaya ya Kilwa, Mwenge ulitembelea, kufungua na kuzindua miradi mitano ya maendeleo yenye thamani ya shilingi 1,900,000,000.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment