Search This Blog

Sunday, October 20, 2019

Ujenzi Hospitali mpya ya Wilaya Nyang'hwale Mkoani Geita wafikia asilimia 82


Katibu Mkuu Dkt. Zainab Chaula ameendelea na ziara yake ya Mikoa ya kanda ya ziwa baada ya kutembelea ujenzi wa Hospitali mpya ya Wilaya ya Nyang'hwale Mkoani Geita ambao umefikia asilimia 82 kisha Kituo cha Afya cha Wilaya hiyo.

Baadae alitembelea ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Chato na kuonekana na kuridhika na kasi ya ujenzi huo huku akiuagiza uongozi wa Wilaya hiyo kuhakikisha ujenzi huo unakamilika kwa wakati na huduma zianze kutolewa.

Dkt. Chaula amemalizia ziara yake mkoani Geita kwa kutembelea ujenzi wa Hospitali mpya ya Rufaa ya Mkoa ambao umekamilika kwa asilimia 79 na kisha baadae kuongea na wafanyakazi wa Hospitali Teule ya mkoa huo.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...