Search This Blog

Thursday, October 17, 2019

Timu ya JWTZ yawasili China, Bendera ya taifa yapandishwa


Timu Teule za Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) zimewasili salama Wuhan nchini China amabapo zinatarajia kushiriki mashindano ya dunia ya majeshi kuanzia tarehe 18 mwezi huu.

Mara baada ya kuwasili, bendera ya Tanzania ilipandishwa kuashiria kuwepo kwa timu za Tanzania kati nchi 110 zinazoshiriki mashindano hayo mwaka huu.

Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa bendera mkurugenzi wa michezo jeshini Kanali Erasmus Bwegoge alisema ni faraja kupandisha bendera ugenini sasa ni wakati muafaka kuitangaza vyema kwa kuibuka na ushindi.

Kwa upande wake mkuu wa msafara Brigedia Jenerali Selemani Mzee amesema kikosi kiko imara na wachezaji wote wako timamu na hakuna majeruhi na wanachoendelea nacho ni mazoezi na kusubiria kupangwa kwa mechi.

Wachezaji wa Tanzania wamekuwa kivutio kila kona huku kaulimbiu ya ‘HAPA KAZI TU’ imekuwa ikitamaniwa kutamkwa na watu mbalimbali wakiwemo wachina huku Rais John Magufuli akiwa kivutio kwa kazi zake nzuri ambazo amekuwa akizifanya kwa maendeleo ya nchi.

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...