Search This Blog
Monday, October 28, 2019
Tiger Woods ashinda taji la 82nd PGA Tour
Tiger Woods amesema kurudi kwake baada ya majeraha na kushinda michuano ya Mabingwa ya Zozo na kusawazisha rikodi ya US PGA Tour kumemaliza kipindi chake cha changamoto kubwa katika kibarua chake hicho.
Woods alimbana kisawasawa Hideki Matsuyama kwenye uwanja wa gofu wa Accordia wa Narashino Country Club na kusawazisha rikodi ya Sam Snead ya 82 na kuwa nafasi ya sita kwenye viwango vya dunia kutoka nafasi ya 10.
Lilikuwa shindano lake la kwanza tangu Wood afanyiwe upasuaji wa goti la kushoto mwezi wa nane na kurejea kwenye mashindano Alhamis akiwa na bogeys tatu mfululizo.
Baada ya ushindi wake wa Augusta, Woods, ambaye pia alifanyiwa upasuaji mara nne wa mgongo, alikosa nafasi kwenye PGA Championship na Open Championship. Woods amesema sasa anatarajia kurejea nchini na kushindana kwenye Olimpiki ya 2020.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment