Search This Blog
Friday, October 11, 2019
Nandy akibadilishana mikataba na uongozi wa Azania Group..
MAKAMPUNI ya Azania Group yanayomiliki Kampuni kubwa ya bidhaa za chakula nchini, leo Oktoba 10, 2019 imezindua sabuni zake mpya za unga ya King Limau na King Marhaba zenye ubora wa kimataifa na kumsainisha mkataba wa kuwa balozi wa bidhaa hiyo mwanamuziki wa Bongo Fleva, Faustina Charles maafuru kama ‘Nandy’.
Wageni waalikwa wakifuatilia yaliyokuwa yakiendelea.
Tukio la kutiliana saini za mkataba wa kuitangaza bidhaa hiyo limefanyika Hoteli ya Hytt Regency, Kilimanjaro Hotel, ambapo Meneja uendelezaji wa kampuni hiyo, Joel Laiser amesema sabuni hizo ni bor, zenye ubunifu na kuondoa kila aina ya uchafu pale zinapotumika.
Laiser amewashauri Watanzania kutumia King Limau na King Marhaba kwa sababu licha ya ubora wake unaojidhihirisha, bado sabuni hizo zinbauzwa kwa bei chee.
Akizungumza mara baada ya kusaini mkataba huo, Nandy alisema kabla ya kuingia mkataba wa kuwa balozi wa sabuni hizo, alianza kuitumia King Limau na King Marhaba kwa zaidi ya wiki tatu na kujidhihirishia ubora wake ndipo akaukubali ubalozi huo.
Nandy alieleza kuwa unapotumia sabuni hizo kufulia hazichubui mikono wala kufubaza nguo kama zingine pia zina harufu nzuri.
Nandy akielezea ubora wa sabuni hiyo baada ya kuitumia kwa wiki tatu kabla kuingia mkataba huo.
“Katika matumizi ya sabuni siku zote mimi huwa napendaga sana yenye harufu nzuri, na hilo ndiyo jambo lililonifurahisha kwenye sabuni hizi,” alisma Nandy.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment