Search This Blog
Friday, October 11, 2019
Aunt atonesha kidonda cha wema!
Ama kweli ule usemi usemao mtoto si nguo umuazime mwenzako una maana kubwa! Staa mkubwa wa filamu za Kibongo, Aunt Ezekiel amemtonesha kidonda shoga’ke, Wema Isaac Sepetu. Aunt amewauliza watu waeleze changamoto za watoto wao wa kwanza kwenye ukurasa wake wa Mtandao wa Instagram na kusababisha minong’ono kwamba huenda alikuwa akimpiga dongo Wema.
Baada ya Aunt kuuliza hivyo ndipo Wema akaibuka na kusema kuwa yeye bado hajapata hivyo hata hajui aandike nini, maneno ambayo yalimchoma kila mmoja na kuanza kumfariji.
“Najua rafiki yangu Wema aliumia sana, lakini sikuwa na maana ya kumuumiza yeye. Nilisahau kabisa kama Mungu hajamjalia, lakini naamini kabisa siku si nyingi Mungu atamsaidia na yeye atapata hitaji la moyo wake,” alisema Aunt. Wema amekuwa akipitia kwenye kipindi kigumu baada ya kujaribu mara kadhaa kutafuta mtoto bila mafanikio
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...

No comments:
Post a Comment