Search This Blog
Thursday, October 24, 2019
Namna Tanzania ilivyopanda viwango vya FIFA
Shirikisho la soka duniani, FIFA, limetoa orodha ya viwango vya soka duniani kwa mwezi Oktoba na kushuhudia Tanzania ikipanda nafasi mbili juu kutoka 135 hadi 133.
Mafanikio hayo yanafuatia ushindi dhidi ya Burundi kufuzu Kombe la Dunia na sare ya 0-0 dhidi ya Rwanda kwenye mechi ya kirafiki ya kalenda ya FIFA.
Tano bora za ukanda wa soka Afrika Mashariki na kati CECAFA, Uganda inaongoza ikifuatiwa na Kenya, Sudan, Rwanda na Tanzania.
Kwa Afrika, Tanzania imepanda nafasi 2 juu kutoka 39 hadi 37, Orodha inayoongozwa na Senegal wakifuatiwa na Tunisia, Nigeria, Algeria na Morocco.
Ubelgiji wao ndiyo vinara wa jumla Ulimwenguni, Ufaransa katika nafasi ya pili, Brazil ya tatu, England ya nne na Uruguay nafasi ya tano.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment