Search This Blog
Thursday, October 24, 2019
Bangladesh: Waliomchoma moto mwanafunzi wahukumiwa kifo
Mahakama nchini Bangladesh imewahukumu kifo watu 16 waliomchoma moto hadi kufa mwanafunzi aliyetoa taarifa ya mwalimu mkuu wake kumnyanyasa kingono.
Nusrat Jahan Rafi, 19, aliyefariki mwezi Aprili mwaka huu katika mji wa Feni, nje ya mji mkuu wa Dhaka nchini humo, aliuawa kwa kuchomwa moto baada ya kutoa taarifa ya kunyanyaswa kingono na mwalimu mkuu wa shule aliyokuwa akisoma.
Mwalimu mkuu aliyetuhumiwa na Nusrat kwa unyanyasaji na wanafunzi wengine wawili wa kike ni miongoni mwa waliohukumiwa adhabu hiyo ya kifo.
Mara baada ya taarifa ya kifo cha binti huyo kusambazwa, ziliamsha mfululizo wa maandamano nchi nzima yaliyokuwa na lengo la kushinikiza Nusrat apate haki.
Walimu watatu wakiwemo mwalimu mkuu, Siraj Ud Doula, ambaye polisi inasema alitoa amri ya kuuwa kwa mwanafunzi huyo akiwa jela baada ya kukamatwa, walipatikana na hatia ya mauaji hayo pia.
Wengine waliopatikana na hatia ni pamoja na Ruhul Amin na Maksud Alam, kiongozi wa Chama Tawala cha Awami League. Maofisa kadhaa wa polisi nao walipatikana na hatia ya kushirikiana na wale waliokamatwa kueneza taarifa za uongo kwamba Nusrat alijitoa uhai.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...


No comments:
Post a Comment