Search This Blog
Sunday, October 20, 2019
Makondakta wa treni wa Ethiopia kwenda China kwa mafunzo
Serikali ya Ethiopia jana iliwaaga makondakta 35 wa treni ambao wanakwenda China kwenye programu ya mafunzo.
Makondakta hao tayari wameshapatiwa mafunzo ya mwaka mmoja nchini Ethiopia na wataalamu wa China na sasa wamepangiwa kupata mafunzo ya miezi sita zaidi kwenye chuo cha Ufundi wa Reli cha Zhengzhou.
Akiongea kwenye hafla ya kuwaaga makondakta hao, Naibu Waziri wa Usafiri wa Ethiopia Awol Wegres amesema serikali ya Ethiopia inapanga kuwezesha mafunzo zaidi katika sekta ya usafiri wa anga na ardhini kwa wataalamu wake kwa ajili ya kuifanya sekta yake ya ugavi kuwa ya kisasa.
China ni muungaji mkono mkubwa wa progranu ya ujenzi wa miundo mbinu ya reli nchini Ethiopia, ikiwa imetoa wataalamu na fedha kusaidia kujenga reli ya umeme yenye urefu wa kilomita 756 na thamani ya dola bilioni 4 za Kimarekani ambayo inaunganisha Ethiopia isiyo na bandari hadi bandari ya Djibout.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment