Search This Blog

Wednesday, October 9, 2019

Kenya yapongezwa mapambano dhidi ya UKIMWI


Mpango wa Umoja wa Mataifa wa kukabiliana na Ukimwi (UNAIDS) hapo jana uliisifu nchi ya Kenya kwa kufanya maendeleo mazuri katika mapambano dhidi ya ugonjwa huo.

Mkurugenzi mpya wa nchi wa UNAIDS, Medhin Tsehaiu  aliwasihi Kenya kuchukua njia za ubunifu ambazo zinavutia zaidi vijana ambao ni idadi ya watu walio katika hatari kubwa.

"Ninapaswa kukupongeza kwa uongozi wako na kujitolea katika juhudi zetu za kumaliza maambukizo ya HIV kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto. Tunashukuru sana kwa msaada wako," Tsehaiu alimwambia mke wa Raisi wa Kenya Margaret Kenyatta wakati walipofanya mazungumzo jijini Nairobi.

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...