Search This Blog

Sunday, October 27, 2019

Karibu watu milioni 1 kukosa huduma za umeme Califonia

Kiasi wakaazi 940,000 wa jimbo la California nchini Marekani wataathirika na kuzimwa kwa huduma za umeme kufuatia upepo mkali kutishia kuangusha nyaya na kusambaza zaidi moto unaoendelea kuwaka kaskazini ya California.

Taarifa iliyotolewa na mamlaka ya nishati ya California imesema hali ya mbaya ya hewa ya upepo mkali inayotajiwa inaleta kitisho katika mfumo wa usambazaji umeme.

Mamlaka hiyo imesema umeme utakatwa kwa awamu katika wiliya zote 36 za jimbo hilo kuanzia siku ya Jumamosi hadi mchana wa kesho Jumatatu. Gavana wa California Gavin Newsom amesema kiasi dola milioni 75 ili kuwasaidia wale watakaoathirika na katizo la huduma za umeme.

Moto mkubwa wa msituni unaendelea kuwaka kaskazini ya California umelazimisha zaidi ya wakaazi 50,000 kuamriwa kuondoka na hali ya upepo mkali unatishia kusambaza zaidi moto huo.

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...