Search This Blog

Tuesday, October 8, 2019

Dkt. Chaula afungua mkutano Wizara ya Afya, TAMISEMI


Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Dkt. Zainab Chaula amefungua mkutano unaojumuisha wizara hiyo, Ofisi ya Rais TAMISEMI, wadau wote wa maendeleo wanaosaidia sekta ya afya pamoja na taasisi za Serikali ambao hufanyika kila mwaka ukiwa na lengo la kujadili mipango ya mwaka mzima.

Katika Mkutano huo unaoendelea Jijini Dodoma, Dkt. Chaula amesema utakua tofauti na mikutano mingine kwasababu unapitia mafanikio na changamoto za mipango mikakati iliyowekwa kwa miaka mitano toka mwaka 2015/16 mpaka ifikapo 2020/21 ikiwa ni pamoja na kuweka maazimio ya pamoja ya kukabiliana na changamoto zitakazobainika ili kufikia malengo yaliyowekwa pia kuandaa mkakati wa tano utakaoanza mwaka 2020/21 mpaka 2025/26.

Awali akizungumza kwenye mkutano huo Mkurugenzi wa huduma za afya, lishe na ustawi wa jamii kutoka ofisi ya Rais TAMISEMI Dkt. Ntuli Kapologwe amesema kuwa madhumuni ya kikao hiki ni kuweka mikakati ya kuhakikisha vituo vya afya vinavyojengwa vinatoa huduma inayostahili na kupunguza vifo vitokana vyo na uzazi.

Kwa upande wa magonjwa yasiyo ya kuambukiza Dkt. Ntuli amesema kuwa Wizara ya Afya kwa kushirikiana na TAMISEMI pamoja wadau watajadili ili kuweza kupunguza athari za magonjwa hayo kwa jamii ili kuweza kuipunguzia Serikali mzigo wa gharama za matibabu.

Mkutano huo unaofanyika kila mwaka ulianza mwaka 1999 na kuendelea mpaka leo ambapo wizara ya Afya kazi yake ni kutunga sera na kuzipeleka Ofisi ya Rais TAMISEMI pamoja na kwa wadau wa maendeleo kwa ajili ili utekelezaji katika mikoa na Halmashauri zote nchini.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...