Search This Blog
Saturday, September 28, 2019
Yanga yadai kuhujumiwa Zambia Wakatiwa Umeme kwa Masaa Manne
Kambi ya timu ya Yanga nchini Zambia imeingia dosari baada ya sehemu waliyofikia umeme kukatika na kupelekea kufanya mazoezi katika eneo la kiza.
Makamu mwenyekiti wa kamati ya Mashindano wa klabu hiyo Saad Kimji amesema kwamba hata kwenye hoteli ambayo wamefikia umeme ulikatika baada ya wao kutua tu sehemu hiyo.
Kimji ameyasema hayo kupitia kipindi cha Duru za Michezo 98.1 Wapo Radio kilichongozwa na Saidally Mwandike ambapo amesema kufuatia swala hilo zahiri kuna dalili za hujuma ambazo zinafanywa na wapinzani wao kuelekea kwenye mchezo wa marudiano klabu bingwa barani Afrika.
Huku akisistiza kuwa wapinzani wao Zesco ni timu ya Shirika la umeme nchini Zambia hivyo huenda ikawa mbinu moja wapo ya kuwavuruga kuelekea kwenye mtanange huo wa siku ya Jumamosi.
Aidha amesema kwamba kwa upande wao kama viongozi wamejipanga kikamilifu kukabiliana na changamoto hizo, huku wachezaji wakiendela kuwa na hamasa ya kutosha kuelekea kwenye mchezo huo.
Yanga SC na Zesco United zinataraji kumenya siku ya jumamosi, ikiwa ni mchezo wa marudiano wa michuano ya klabu bingwa Afrika huku wanajangwani hao wakiwa na kumbukumbu ya kutoka sare ya bao 1 – 1 kwenye mechi ya awali iliyopigwa katika dimba la Mkapa jijini Dar Es Salaam.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment