Search This Blog
Tuesday, September 10, 2019
Viongozi wanaotoa ahadi hewa, waandaliwa mkakati
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk. Damas Ndumbaro amesema serikali imekuwa ikifanya vikao vya majadiliano kuhusu viongozi mbalimbali wanaokuja nchini kutoka nje na kutoa ahadi bila kuzitekeleza ili kufikia muafaka.
Dk. Ndumbaro ameyasema hayo, bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu, Tauhida Cassian, maelezo ya serikali juu ya viongozi hao wanaokuja nchini.
“Je, serikali ina maelezo gani juu ya viongozi wanaokuja Tanzania na kutembelea baadhi ya maeneo na kisha wanapokuta miradi ya wananchi huahidi kusaidia na baadaye kushindwa kutimiza ahadi zao,” amehoji mbunge.
Akijibu swali hilo, Dk. Ndumbaro amesema ahadi ambazo hutolewa na baadaye kushindwa kutimizwa wizara huratibu vikao vya majadiliano vinavyoshirikisha wahusika pamoja na wizara za kisekta na taasisi za kiserikali ili kupata muafaka juu ya suala husika.
“Tanzania imekuwa ikipokea viongozi wageni kutoa nje ya nchi katika makundi mawili, yaani viongozi hao hutembelea kwa safari za kiserikali na binafsi ambapo hupata fursa ya kuona miradi ya wananchi.
“Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikaino wa Afrika Mashariki, ina jukumu la kuratibu na kusimamia safari za kikazi kutoka mataifa ya kigeni ikiwa ni pamoja na kufuatilia utekelezaji wa ahadi mbalimbali zinazotolewa na viongozi hao kwa kushirikiana na wizara za kisekta na taasisi kiserikali,” amesema.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment