Search This Blog
Thursday, September 5, 2019
Tessy Atoa Kauli Tata Kumhusu Aslay
MREMBO Tessy Abdul ‘Tessy Chocolate’ ametoa kauli tata inayotafsiri kwamba anamzungumzia mzazi mwenziye, Aslay Isihaka japokuwa hakutaka kumtaja moja kwa moja.
Akizungumza mawili-matatu kuhusu maisha yake kwa jumla mbele ya kinasa sauti cha Amani, Tessy alichomekea kuwa, watu wasiwe na wasiwasi pindi inapotokea wamepoteza kitu maishani kwani yeye amejifunza kama Mungu akipanga utakuwa na kitu hata kama kikipotea ipo siku kitarudi tu.
“Watu wengi utakuta wakilaumu vitu mbalimbali kwenye maisha yao vikiondoka, lakini wanasahau kuwa kitu kama kikiondoka kwenye maisha yako na hakikurudi tena, basi Mungu amepanga, lakini kama alisema ni chako, kitarudi tu bila tatizo lolote,” alisema Tessy huku akiachia tabasamu na alipoulizwa kama kauli hiyo inamaanisha anaweza kurudiana na Aslay hakutaka kuweka wazi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...
No comments:
Post a Comment