Search This Blog
Sunday, September 22, 2019
Takukuru Manyara yazidi kukamata wala Rushwa
Na John Walter-Manyara
Mkuu wa Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa mkoani Manyara Fidelis Kalungura, amesema kuwa wanaendelea na mapambano hayo ili kuhakikisha yanapungua au kumalizika kabisa huku wakiwachukulia hatua kali za kisheria wananchi na viongozi wanaojihusisha na vitendo hivyo katika jamii.
Amesema ofisi yao kwa kushiriana na ofisi ya mashtaka inatarajia kumfikisha Mahakamani Bi Justina Patrick Gidohay kwa makosa mawili ambayo ni ubadhirifu wa mali ya Umma kinyume cha kifungu cha 28 (1) cha sheria ya kuzuia na kupambana na Rushwa Namba 11/2007 na kuisababishia serikali hasara ya shilingi 2,241,400/= kinyume na Aya ya 10 (1) ya jedwali la kwanza la kifungu Namba 57 (1) na 60 (2) vyote vya sheria ya uhujumu uchumi sura ya 200 ya mwaka 2002.
Awali Takukuru ilipokea taarifa kwamba Bi Justina Patrick ambaye alipewa majukumu ya kukusanya fedha za bili ya maji toka kwa wateja mbalimbali kwa kipindi cha mwaka 2013/2014 aliweza kukusanya pesa za malipo ya bili za maji kiasi cha shilingi 2,241,400/= na kuzifanyia ubadhirifu badala ya kuzipeleka benki.
Wakati huo huo Takukuru mkoani hapa inajiandaa kumfikisha mahakamani Mratibu wa Kinga na Chanjo wilaya ya Simanjiro Ezekiel Fabian Mayumba kwa kughushi .
Mkuu wa Takukuru Manyara Fidelis Kalungura alisema katika nyaraka za marejesho ya matumizi ya fedha za Chanjo ya Surua Rubella,kiasi cha Shilingi 75,396,000/= mtuhumiwa aliwasilisha nyaraka za kughushi malipo ya shilingi 6,166,000/= kwa madai kuwa ni malipo kwa ajili ya viburudisho,maji na chakula kwa washiriki wa semina ya chanjo ya surua Rubella huku akijua kuwa hakuna semina iliyofanyika.
Kalungura amesema mtuhumiwa atafikishwa mahakamani kwa makosa yafuatayo ,moja ya kughushi kinyume na vifungu namba 333, 335 (a) na 137 vya kanuni ya adhabu sura ya 16, Mbili,Kuwasilisha nyaraka yenye maelezo ya uongo aliyoyaandika yeye mwenyewe kwa mkono wake kitendo ambacho ni kosa chini ya kifungu cha 22 cha sheria ya kuzuia na kupambana na Rushwa namba 11 ya mwaka 2007, Tatu,Kufanya ubadhirifu wa mali ya Umma kiasi cha sjilingi 6,166,000/= kitendo ambacho ni kosa chini ya kifungu cha 28(1) cha sheria ya kuzuia na kupambana na Rushwa namba 11 ya mwaka 2007.
Takukuru mkoani Manyara inaendelea kutoa wito kwa wananchi kuendeleza mapambano dhidi ya Rushwa kwa kukataaa kutoa na kupokea rushwa,kutoa taarifa wanapoona vitendo hivyo vinavyokea au kutaka kutokea katika ofisi za Takukuru au kupiga simu ya bure 113 wakati wowote.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...
No comments:
Post a Comment