Search This Blog
Thursday, September 26, 2019
Serikali kuendelea kuboresha mazingira ya uwekezaji nchini
Na Ahmad Mmow, Lindi
Serikali imesema kutokanana kutambua na kuthamini mchango wa wawekekezaji katika kuchangia ukuaji wa uchumi itaendelea kuboresha mazingira ya uwekezaji nchini.
Hayo yameelezwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji, Angela Kairuki. Alipozungumza kwenye mkutano wa mashauriano baina ya serikali, wawekezaji na wafanyabiashara waliopo katika mkoa wa Lindi. Ambao ulifanyika katika manispaa ya Lindi.
Waziri Kairuki alisema serikali itaendelea kuboresha mazingira ya uwekezaji na biashara na kushughulikia kutatua kero na changamoto mbalimbali zilizopo katika sekta hizo ili kuhakikisha kunakuwepo mazingira bora zaidi kwa uwekezaji na biashara.
Alisema kwa kuzingatia ukweli huo na nia thabiti iliyo njema kwa wawekezaji na wafanyabiashara nchini, inatarajia kupeleka mswada maalumu bungeni kwaajili ya kuboresha mazingira ya uwekezaji na biashara. Mswaada ambao utakuwa na marekebisho mbalimbali yanayohusu biashara na uwekezaji.
Waziri Kairuki aliendelea kuwatoa hofu wawekezaji kwa kusema kwamba mbali na kupeleka mswada huo bungeni, lakini pia kutakuwa na mabadiliko ya sheria ya uwekezaji. Kwahiyo kabla ya kufika mwaka ujao kutashuhudiwa mabadiliko. Ikiwamo kituo cha uwekezaji( TIC) kuongezwa nguvu ili kiweze kuwa na maamuzi makubwa yenye tija kwa wawekezaji na taifa.
Sanjari na hayo, waziri huyo mwenye dhamana ya uwekezaji alibainisha kwamba serikali itaendelea kufanya mapitio ya sera ya uwekezaji. Kwahiyo wasisite kujisajili kwenye kituo cha uwekezaji, kwani mikakati iliyopo itakuwa na tija kubwa kwao.
Aidha waziri Kairuki alionya kwamba serikali haitasita kumchukulia hatua za kisheria yeyote atayeendelea kutoza kodi zilizofutwa au mambo yaliyopata msamaha. Akiweka wazi kwamba kuendelea kufanya kilichokatazwa ( kutoza kodi zilizoondolewa) ni kosa.
"Wakuu wa taasisi, hasa watendaji shukeni chini ili muwalee wawekezaji na wafanyabiashara kwa kuwafundisha na kuwasaidia jinsi ya kutatua changamoto zilizopo kwenye shughuli zao," aliagiza Kairuki.
Katika hali inayodhihirisha serikali imeamua kwa dhati kuvutia wawekeji nchini, waziri huyo amezitaka halmashauri nchini zitenge bajeti kwa ajili ya maeneo ya uwekezaji. Kwani zinatakiwa kutenga maeneo yatayotumika kwa shughuli hiyo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment