Search This Blog
Thursday, September 26, 2019
Mama Wajawazito waaswa kutokimbilia kwa waganga wa kienyeji
Na Rahel Nyabali, Tabora
Wakati Serikali ikiendelea na mikakati mbalimbali ya kupambana kupunguza vifo vya mama na mtoto kwa kuboresha sekta ya Afya na kutoa elimu kwa wananchi, Wakina mama Wajawazito wametakiwa kuacha tabia ya kukimbilia kwa wakunga wa jadi ama waganga wa kienyeji pindi wanapotaka kujifungua kwani ni kuhatarisha usalama wa Afya zao.
Wito huo umetolewa na Mganga Mkuu wilayani Kaliua Mkoani Tabora, Charles Canrad amesema Wajawazito kukimbilia kwa wakunga wa jadi na waganga wa kienyeji ni miongoni mwa sababu zinaweza kusababisha athari kwa mama mjamzito na mtoto ikiwa ni pamoja na kushindwa kufika katika vituo vya kutolea huduma za Afya na kupelekea kifo.
Charles amesema ili kukabiliana na tatizo hilo wilayani wilayani humo imezidi kuboresha huduma za Afya ambazo zitasaidia kupunguza changamoto ya vifo vya mama na mtoto Halmashauri ya wilaya ya Kaliua imeongeza nguvu zaidi katika ujenzi wa Zahanati ambapo nne zimekamilika.
Mary Juma ni Mkazi wa Kijiji cha Zugimlole amesema ujenzi wa Zahanati hizi umesaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza tatizo la akina mama kwenda kupata huduma kwa waganga wa kienyeji na wakunga wa jadi pindi wanapotaka kujifungua ingawa ombi lao kubwa ni kuongezwa kwa wataalamu wa Afya katika Vituo vya kutolea huduma.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment