MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Samatta amefichua kuwa alitamani kuona timu yake inapangwa na klabu ya Barcelona au Real Madrid katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Hivi karibuni timu ya Samatta, Genk ilipangwa kundi moja na Liverpool kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Samatta ambaye ni nahodha wa Taifa Stars na mshambuliaji wa KRC Genk ya Ubelgiji ametoa kauli hiyo baada ya timu yake kupangwa kwenye Kundi H, wakiwa na Liverpool, Red Bull na Napoli.
Akizungumza na Championi Ijumaa, Samatta alisema
kuwa alitamani kuona wakipangwa na timu hizo za Hispania ili kuweza kutimiza ndoto yake lakini kwa kuwa wameangukia kwa Liverpool haoni shida yoyote.
“Kwanza nilitamani kuona tunapangwa na Barcelona au Real Madrid hiyo ndiyo ingekuwa furaha yangu kuona naweza kucheza dhidi ya timu hizo katika michuano hiyo lakini tumeangukia kwa Liverpool siyo mbaya japo uwanja wao umekuwa mgumu.
“Lakini niseme kwamba ukiangalia kwenye kundi letu sisi ndiyo wadogo peke yetu katika historia ya michuano hii, watu lazima waelewe kwa sababu Genk ina muda mrefu hajashiriki hivyo tumeingia kama wageni ambao tunahitaji kupata uzoefu mkubwa,” alisema Samatta
Search This Blog
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment