Search This Blog
Wednesday, September 18, 2019
Ofisi ya Klabu ya riadha Babati,Garmaa Athletic kufunguliwa wikiendi hii
Na John Walter-Babati
Mashindano ya riadha ya kwa rika zote yanatarajiwa kufanyika tarehe 21.9.2019 Mjini Babati katika uwanja wa Kwaraa katika Mita 2.5, Kilomita 5 na Kilomita 10 ikiwa ni sambamba na ufunguzi wa Ofisi ya Garmaa Athletic Club.
Akizungumza na Muungwana Blog Mkurugenzi wa taasisi ya ‘Garmaa Athletic ’ inayoandaa mashindano hayo, Abdalah Magubika, alisema wameamua kuandaa mashindano hayo ili kukuza mchezo wa riadha kwa mkoa wa Manyara na kuzindua rasmi ofisi hizo ili kuendelea kuupa heshima Mchezo huo hapa nchini.
Alisema mbio hizo ni moja ya chachu ya kuwaandaa wanariadha wengine wa baadae watakaoipeperusha vyema bendera ya Tanzania kama ilivyo kwa akina Alphonce Simbu na wengine.
Alisema mchezo wa riadha kwa sasa unakuwa kwa kasi kubwa ukichagizwa na wanariadha maarufu kutoka katika mkoa wa Manyara.
Kuhusu Maandalizi Magubika , amesema mpaka sasa yanaendelea vizuri hivyo yataanza saa 1:00 asubuhi hadi majira ya mchana.
Hata hivyo amewashukuru wadau wa Michezo waliojitokeza kutoa michango yao ili kuhakikisha mbio hizo zinafanikiwa kufanyika.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment