Search This Blog
Sunday, September 8, 2019
Namna ya Kujitibu Maumivu ya Korodani Nyumbani
Maumivu ya korodani ni tatizo linalowasumbua sana wanaume wengi, kawaida maumivu ya korodani hutokea katika korodani moja au zote mbili endapo zitaumizwa kwa kuumia au maambukizi.
Maumivu hayo husababishwa na mambo mbalimbali yakiwemo; maambukizi ya bacteria au magonjwa ya zinaa, kutokunywa maji mengi, misuguano inayoathiri moja kwa moja ngozi na mirija ya ndani ya korodani ambayo inaweza kusababishwa na uvaaji wa nguo za ndani zinazobana sana, kujikusanya kwa maji na uchafu, ngiri, saratani ya korodani au sababu za kupata ajali.
Hivyo endapo utapata maumivu ya korodani zipo namna kadhaa ambazo mwanaume anaweza kujipatia huduma ya kwanza akiwa nyumbani kama namna ya kutibu maumivu hayo.
Hivyo kama upo nyumbani inashauriwa na madaktari kujitibu kwa kujitahidi kunywa maji mengi na kutotunza mkojo, lakini pia hakikisha unapangusa eneo la korodani zako kwa dakika 5 kwa kutumia maji ya barafu au hata barafu yenyewe.
Pia kwa wale wasio na uwezo wa kupata maji ya barafu chemsha maji yawe vuguvugu kisha weka chumvi kidogo, jikande taratibu kwa dakika 5.
Baada ya kufanya hivi endapo maumivu bado yanasumbua basi fika hospitalini haraka ili ufanyiwe uchunguzwe na kusaidiwa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment