Search This Blog

Sunday, September 8, 2019

Meya wa Ilala kukarabati Shule ya Bunge



Na Heri Shaaban.

Meya wa Manispaa ya Ilala, Omary Kumbilamoto amesema ofisi yake inatarajia kukarabati  shule ya Msingi Bunge iliyopo wilayani Ilala.

Meya Kumbilamoto aliyasema hayo Katika mahafali ya 25 ya shule hiyo ambapo jumla ya wanafunzi 300 walipewa vyeti.

"Shule hii kongwe  nawaidi wazazi  ofisi yangu ya Meya itabeba jukumu ili la kuboresha mazingira ya shule kwa kushirikiana na Mbunge wa Ilala Mussa Zungu"alisema Kumbilamoto.

Meya kumbilamoto amemwagiza Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Bunge kuandika barua ya maombi yanayoitajika katika shule hiyo na kuweka mchanganuo ili changamoto iweze kutatuliwa.

Alisema Rais wa awamu ya tano amewekeza katika sekta ya elimu na kauli mbiu yake elimu bure hivyo wazazi tutumie nafasi hiyo kwa ushirikiano wa Walimu katika kukuza taaluma na kuongeza ufaulu wilaya Ilala.

Meya alisema Wilaya ya Ilala kila mwaka  inafanya vizuri matokeo ya elimu ya msingi katika ufaulu Ilala inajivunia inashika nafasi za kwanza hadi Taifa  na mwaka huu itafanya vizuri zaidi watoto wameandaliwa vizuri.

Aidha alisema awali shule za kata wazazi walikuwa wanaogopa kupeleka watoto wao kusoma sekondari katika awamu ya tano mazingira ya shule hiyo yameboreshwa kiwango cha ufaulu kimeongezeka katika shule 100 shule 50 za sekondari za kata zimepata alama za juu.

Kwa upande wake Katibu wa Mbunge wa Ilala  Busoro Pazi alimuomba Mwalimu wa Shule hiyo apeleke barua ya kuelezea changamoto za shule pesa za Mfuko wa Jimbo la Ilala zikifika Mbunge Mussa Zungu na Meya watatatua kero.

Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Bunge Radhia Mfalingundi alisema shule ilianzishwa 1957  ikijulikana kwa jina la  Bortoni  Mwaka 1963 shule ilikuwa ikimilikiwa na halmashauri ya Jiji na Lugha ya kufundishia kiswahili.

Akielezea mafanikio Mwalimu Radhia alisema shule hiyo kwa upande wa taaluma kila mwaka   inafanya vizuri kutokana na mikakati ya wazazi , walimu na uongozi wa shule kwa kuakikisha kila mwanafunzi anafaulu vizuri.

Akizungumzia mafanikio alisema mwaka 2018 darasa la saba 240 waliofanya mitihani 238 waliochaguliwa 232 sawa na asilimia 97 ,4 ya ufaulu na mitihani ya kujipima darasa la nne  2018 wanafunzi wote walifaulu kwa alama A,B na C.

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...