Search This Blog

Wednesday, September 11, 2019

Mbosso ashusha waraka mzito kufuatia kifo cha Mchekeshaji kutoka 'Cheka TU'


Kufuatia kusambaa kwa taarifa ya kifo cha Mchekeshaji aliyepata umaarufu kupitia kipindi cha Cheka Tu kinachoongozwa na Coy Mzungu, Boss Matha. Msanii kutoka lebo ya WCB, Mbosso amefunguka maneno mazito.

Mbosso kupitia mtandao wa Instagram ameandika, "Licha ya Vipingamizi Vingi juu ya Mimi kuwa na Wewe takribani au ndani ya zaidi ya Miaka Mitano (5) iliyopita, hatukuacha kuonyeshana ni kiasi gani tulikuwa tunahitajiana sana kwenye Safari yetu ya maisha."

"Japo jitihada zetu hazikuweza kufanikisha Mimi na wewe Kuwa Pamoja .., ila mbegu tuliyoipanda vuno letu ulichagua Liwe siri baina yangu Mimi na wewe.., sikukubishia japo Mwazoni nilikukatalia kwa sababu 'najijua kifua cha Kuficha Siri sina..' , ila nikakuahidi sitadiriki kuitoa Popote na hata waliotuhisi tulikuwa tunawakatalia.., iwe Faragha au mbele ya hadhira tulitamka Sio Kweli, Hapana, Hakuna Kitu Kama hicho..' Hayo ndo yalikuwa Majibu Yetu."

 "Sasa Umeondoka bila kunipa ruksa juu ya hili Je, niendelee kuitunza hii siri .., na Je, anavyoendelea Kukua akija kuniuliza na nikwambia Mama alisema uwe siri atanielewa Kweli ''.." ?.. Wallah Moyo wangu unauma Martha , hukupaswa kuondoka wakati huu, Mapema mno Dah ..!! "Nenda Martha Mwingi Furaha na Ucheshi , Hata Mama Kasema Leo Msiba..:, ' jana ulikuwa unatabasamu hadi ulipofumba Macho , "Innalillah Wainnailaih Raajuun " ..' Mwenyezi Mungu akupe Kauli thabiti inshaallah.., ' Lala salama Martha."

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...