Search This Blog
Sunday, September 15, 2019
Kocha wa Zamani wa Taifa Stars Afariki Dunia
Kocha wa zamani wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars Mjerumani Rudolf ‘Rudi’ Gutendorf amefariki dunia akiwa ana umri wa miaka 93 jana.
Taarifa ya familia yake nchini Ujerumani imesema kwamba Gutendorf aliyeweka rekodi ya dunia ya kufundisha timu nyingi zaidi duniani, 55 katika nchi 32 za mabara matano amefariki dunia jana.
Makamu wa Rais wa Chama cha Soka Ujerumani, Dk Rainer Koch alimpe heshima ya “Balozi Bora wa Soka ya Ujerumani”.
Kwa mara ya mwisho Gutendorf alifundisha kikosi cha timu ya taifa ya Samoa mwaka 2003 baada ya kuweka pia rekodi ya kuwa kocha wa kwanza wa kigeni kutwaa taji la Ligi Kuu ya Japan mwaka 1984 akiwa na klabu ya Yomiuri SC.
Nchini Tanzania atakumbukwa zaidi alipoiwezesha Bara kufika fainali ya michuano hiyo mwaka 1981 mjini Dar es Salaam na kufungwa na Kenya Novemba 28, bao pekee la James Ouma dakika ya 22.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment