MSHAMBULIAJI wa Simba, Meddie Kagere, amesema kitendo cha timu yake kufunga idadi ndogo ya mabao kinatokana na kumkosa nahodha wa timu hiyo, John Bocco ambaye ni majeruhi.
John Bocco mpaka sasa hajafanikiwa kucheza mchezo wowote wa Ligi Kuu Bara kutokana na majeraha aliyoyapata wakati wa mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Azam FC.
Kagere ameliambia Championi Jumatano kuwa, japokuwa Simba ina wachezaji wengi katika safu ya ushambuliaji, lakini kukosekana kwa nyota huyo ni pigo kwake kwani ana msaada mkubwa katika eneo la ushambuliaji.
“Simba ina wachezaji wengi sana wazuri ambao wanaweza kucheza katika eneo la ushambuliaji, lakini kukosekana kwa nahodha wetu John Bocco katika michezo iliyopita imetupunguzia vitu kama muunganiko mzuri ambao yeye akiwepo huchangia upatikanaji wa mabao mengi,” alisema.
Kagere mpaka sasa kwenye mechi mbili za ligi amefunga mabao matatu ambapo mawili aliyafunga walipoifunga JKT Tanzania mabao 3-1, kisha katika ushindi wa 2-1 dhidi ya Mtibwa, alifunga moja.
Search This Blog
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment