Search This Blog
Saturday, September 7, 2019
DC Muro agusa maisha ya Walemavu
Mkuu wa wilaya ya Arumeru Ndugu Jerry Muro kwa kushirikiana na Taasisi ya walemavu wa Uti wa mgongo KASI imetoa misadaa mbalimbali kwa walemavu wenye matatizo ya Uti wa Mgongo walioko katika wilaya ya Arumeru.
Dc Muro ambae ameamua kuonyesha juhudi binafsi katika kuwasaidia watu wenye ulemavu amesema wametoa misaada ya kuanza maisha ya Ujasiriamali kwa watu wenye ulemavu ili waweze kumudu maisha hatua itakayowasaidia kuwaondoa katika kundi la utegemezi katika familia.
Huku akisema jambo linalochangia watu kuwanyanyapaa ambapo ametoa misaada mbalimbali ya kuanzisha biashara ndogondogo ikiwemo uuzaji wa vifaa vya ujenzi, vyombo vya majumbani, miradi ufugaji kuku, miradi ya ufugaji mbuzi na miradi ya uuzaji maji ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono serikali ya awamu ya tano chini ya Mhe, Rais, Dkt. John Pombe Magufuli
Aliongeza kusema kuwa kwa kuendelea kuwajali watu wenye ulemavu hatua inayowasaidia kuwajengea uwezo wa kupambana na changamoto walizonazo ambazo zinawafanya kuwa tegemezi kwenye jamii.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...


No comments:
Post a Comment