Search This Blog

Saturday, September 7, 2019

Rose Muhando aibuka na 'Walionicheka'


Mwimbaji Mkongwe wa nyimbo za Injili nchini, Rose Muhando ameibuka na kutoa wimbo mpya uitwao 'Walionicheka' ambao unatamba kwasasa kwenye anga za muziki wa aina hiyo.

Rose ametoa wimbo wake huo jana Alhamisi ambao amemshirikisha mwanamuziki kutoka Kenya, Ring Tone ambaye pia huimba muziki wa aina hiyo.

Kwenye wimbo huo Rose amemshukuru Mungu kwa kumvusha katika kipindi kigumu alichopitia kwani mwaka jana mwimbaji huyo akiwa nchini Kenya alipata matatizo ya kiafya ikiwemo kukumbwa na mapepo.

Rose amewahi kutamba na nyimbo kama Mteule uwe Macho, Yesu Nakupenda, Tabu Zangu, Wambea Nao, Uko Wapi na nyingine nyingi.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...