Search This Blog
Tuesday, September 10, 2019
Chuo Kikuu cha Zimbabwe kimeahirisha Mahafali kufuatia kifo cha Mugabe
Chuo Kikuu cha Zimbabwe kimeahirisha hafla ya kuhitimu ambayo ilikuwa imepangwa kufanyika Septemba 14 na wiki moja kufuatia kifo cha rais wa zamani Robert Mugabe.
Katika taarifa kwa waandishi wa habari iliyotolewa Jumanne na idara ya habari na uhusiano wa umma, chuo kikuu kinachoongoza nchini kimesema kuwa sherehe ya kuhitimu sasa itafanyika Septemba 20 mwaka huu.
Serikali tayari imetangaza kuwa Mugabe, aliyefariki akiwa nchini Singapore mnamo Septemba 6, atazikwa siku ya Jumapili, Septemba 15, ingawa haikuonyesha ni wapi mazishi hayo yatafanyika.
Kumekuwa na ripoti kwamba Mugabe, ambaye alijiuzulu kama Rais mnamo Novemba 2017, alikuwa amesema kuwa hataki kuzikwa kwenye "National Heroes Acre" mjini Harare.
Familia yake bado haijathibitisha tarehe ya mazishi na msemaji wa familia Leo Mugabe aliwaambia wanahabari kwamba viongozi wa jadi katika kijiji cha Zvimba ambako nyumbani kwa Mugabe watatangaza juu ya suala hilo
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment