Search This Blog
Monday, September 16, 2019
Binti aliyedaiwa kupewa mimba amkana mwalimu Mkuu
Mahakama ya hakimu mkazi Mkoa wa Kigoma imemwachia huru mwalimu Mkuu wa Shule ya msingi Nyantore iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma baada ya upande wa mashtaka kuomba kutoendelea na shauri hilo kufuatia shahidi wa pili mwanafunzi mwenye mimba kueleza mbele ya mahakama kuwa hamfahamu mtu aliyeshiriki naye mapenzi hadi kupata mimba.
Aidha shahidi huyo amekana kuwa na umri wa miaka 16 kama upande wa mashtaka ulivyosema kupitia upelelezi wa polisi na kwa mujibu wa baba wa mwanafunzi huyo amesema binti yake ana umri wa miaka 19 na kwa muda mrefu Polisi walikuwa wakimshawishi aseme ana miaka 16 tofauti na anavyofahamu.
Kesi hiyo kwa mara ya kwanza ilisomwa Agosti 14 ambapo shahidi wa kwanza mama mzazi wa mwanafunzi huyo Sakina Kazili (55) aliiambia mahakama hiyo Septemba 12 kuwa binti yake ana miaka 16 na kwamba alizaliwa Februari 7, 2003.
Hakimu mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu mkazi, Flora Mtarania amesema anakubali ombi la upande wa mashtaka kufuta shauri na kwamba haizui kumkamata mtuhumiwa mwalimu mkuu huyo, Jason Rwekaza iwapo baadae itabainika kuwepo sababu za kufanya hivyo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment