Search This Blog
Monday, September 16, 2019
Azam FC kuifuata Triangle United kwa mtindo huu
Kikosi cha Azam FC kinatarajia kuondoka Septemba 22, 2019 kwenda nchini Zimbabwe kwaajili ya mchezo wa marudiano wa Kombe la Shirikisho barani Afrika dhidi ya Triangle United ya huko utakaopigwa Septemba 28, 2019.
Afisa Habari wa timu hiyo Jaffer Idd Maganga amesema timu hiyo itaondoka kwa mafungu ambapo kundi la kwanza litahusisha wachezaji ambao hawatakuwa kwenye majukumu ya timu ya taifa (Taifa Stars) itakayokuwa dimbani Septemba 21 kukabiliana na Sudan katika mchezo wa kufuzu CHAN.
Kundi lingine litaondoka Septemba 23 likihusisha wachezaji waliokuwa kwenye majukumu ya timu ya taifa pamoja na kocha Etienne Ndayiragije ambaye pia anakaimu nafasi ya kocha mkuu wa timu hiyo ya taifa.
Katika hatua nyingine uongozi wa Azam FC umewashukuru Watanzania wote kwa umoja waliouonesha na kuujaza uwanja wa Chamazi katika mchezo wa kwanza huku ukiomba radhi kwa matokeo mabaya.
“Tunajua tumewaangusha sana Watanzania kiujumla kwa aina ya matokeo tuliyopata, lakini haikuwa nia yetu, bali ni sehemu ya matokeo ya soka," alisema.
Huu sio mwisho wa vita, ndiyo kwanza dakika 90 za mwanzo zimemalizika, tumegundua tulipoteleza na sasa tumeanza kujipanga vilivyo kuelekea dakika 90 nyingine zijazo ugenini”.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment