Search This Blog
Wednesday, August 28, 2019
Waziri Jafo Atangaza Majina ya Wanafunzi Waliochaguliwa Kujiunga Na Kidato Cha Tano Awamu Ya Pili 2019
Serikali imewachagua wanafunzi 1,674 kujiunga kidato cha tano baada ya awamu ya kwanza kukosa fursa hiyo.
Katia uchaguzi wa Awamu ya kwanza, serikali ilitangaza kuwa wasichana wote waliofaulu kidato cha nne walichaguliwa kujiunga vyuo mbalimbali pamoja na kidato cha sita lakini wavulana 1,861 hawakuchaguliwa licha ya kuwa na sifa.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Selemani Jafo ametangaza hayo leo, Jumatano (Agosti 28, 2019), jijini Dodoma huku akisema kuwa 187 wamekosa kwa kukosa uwiano katika tahasusi zao.
Waziri Jafo amesema wanafunzi hao wanatakiwa kuanza kuripoti katika shule walizochaguliwa kuanzia Septemba 2 hadi 16,2019 huku akiwataka waliokosa nafasi kutokata tamaa badala yake waombe vyuo vya kati ili wajiunge.
Ametaja sababu za kupatikana kwa nafasi ni kutokana na baadhi ya wanafunzi kujiunga shule binafsi na baadhi ya shule zimeongeza majengo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment