Search This Blog

Saturday, August 10, 2019

Watumishi watakiwa kufanya kazi bila kusukumwa


Watumishi wa hospitali ya rufaa ya mkoa wa iringa wametakiwa kufanya kazi kwa kujituma bila kusukumwa na mtu yeyote.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa idara ya tiba kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto Dkt.Grace Magembe wakati akiongea na watumishi wa hospitali hiyo ikiwa ni ziara ya kujionea huduma za kibingwa zilizofanywa katika hospitali hiyo ambazo zimetolewa na madaktari bingwa kutoka wizarani.

Dkt. Magembe alisema kuwa amepokea majina ya Watumishi ambao wamepewa onyo mara kadhaa na wameshindwa kubadilika hivyo watachukuliwa hatua kulingana na taratibu za kiutumishi.

”Wengine mtapewa muda wa kujirekebisha na kufuatiliwa kuona kama mmebadilika,sitegemei kufukuza mtaalam yeyote kwani wanayo nafasi ya kubadilika”.

“Kama mtumishi wa umma na ulipewa viapo hivyo mnapaswa kufanya kazi bila kusukumwa kwani kwenye utumishi wa umma hakuna kubebana”.Alisisitiza Dkt.Magembe.

Aidha, alisema kuwa wananchi wanawategemea wataalam hao katika kutoa huduma za afya zinazostahili.

“Mgonjwa anapokuja hospitali ya rufaa ya mkoa anatakiwa kuona mabadiliko kuanzia lugha nzuri na huduma kwa mteja izingatiwe, lazima utofauti uwepo wa hospitali ya mkoa na vituo vya huduma vilivyopo chini,”alisema Dkt.Magembe.

Akitoa ripoti ya huduma za kibingwa zilizofanywa na madkatari hao Mganga Mfawidhi wa hospitali ya rufaa ya mkoa wa dodoma ambaye ni mwenyekiti wa waganga wafawidhi Tanzania bara Dkt. Ibenzi Ernest alisema tangu huduma hizo kutolewa mwishoni mwa mwezi wa saba mwaka huu wamewaona wagonjwa 656,wagonjwa 41 wamefanyiwa vipimo na wagonjwa 88 wamepata huduma za upasuaji.




No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...