Search This Blog
Thursday, August 1, 2019
Watu 20 wafariki kutokana na mafuriko
Takriban watu 20 wamefariki na wengine kadhaa kujeruhiwa baada ya mvua kusababisha mafuriko na uharibifu mkubwa katika mji wa bandari wa Karachi kusini mwa Pakistan katika kipindi cha siku tatu zilizopita.
Vifo vingi vilitokea kwa sababu ya umeme, ajali za barabarani na tukio la kuanguka kwa paa. Wakuu wa jiji pia wametangaza majengo kadhaa kuwa hatari, na kuwataka wakaazi waondoke kwani zinaweza kuporomoka kutokana na mvua kubwa.
Kulingana na takwimu za hivi karibuni zilizotolewa na Mamlaka ya Usimamizi wa Maafa nchini humo, jumla ya watu 83 walifariki na wengine 74 kujeruhiwa kutokana na ajali tofauti zinazohusiana na mvua nchini kote kutoka Julai Mosi hadi Julai 25 mwaka huu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...


No comments:
Post a Comment