Search This Blog

Tuesday, August 6, 2019

UGANDA: Bobi Wine kuburuzwa mahakamani kwa tuhuma za kumkera na kumkejeli Rais Museveni



Msanii wa muziki nchini Uganda, Robert Kyagulanyi maarufu maarufu kwa jina la Bobi Wine ameshtakiwa nchini humo kwa tuhuma za kumkera na kumkejeli Rais wa taifa hilo, Yoweri Museveni.



Mashtaka hayo, Yanajumuishwa na tukio la Agosti mwaka Jana, Ambapo Bobi Wine alishutumiwa kuongoza maandamano sehemu ambayo gari la Rais Museveni lilipigwa mawe na Wafuasi wa Bobi Wine.

Mbunge huyo wa Jimbo la Kyadondo Mashariki, Tayari anakabiliwa na shtaka la uhaini na anaweza kufungwa kifungo cha maisha iwapo atapatikana na hatia.

Mapema mwezi Julai mwaka huu, Bobi Wine alitangaza kuwa atawania Urais wa Uganda dhidi ya Rais Museveni katika uchaguzi Mkuu wa mwaka 2021.

Chanzo: Daily Monitor.

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...