Search This Blog
Tuesday, August 13, 2019
Serikali yawataka wananchi kulinda rasilimali za Madini
Waziri wa Madini, Dotto Biteko amewataka wananchi kulinda rasilimali za madini nchini ikiwa ni pamoja na kutumia utajiri wa madini uliopo kubadilisha maisha yao.
Biteko ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Pachani Wilaya Nanyumbu Mkoani Mtwara, juu ya kusitishwa kwa shughuli ya uchimbaji wa madini ya chuma iliyokuwa inaendea Kijiji hipo.
Amesema kuwa kwa miaka mingi utajiri wa madini yaliyopo nchini yalikuwa yakiwanufaisha wageni huku wenyeji wakiwa bado wanabaki masikini licha ya rasilimali hizo kuwepo kwenye maeneo yao.
“Tanzania ni moja kati ya nchi tajiri kwa madini duniani, hata kwa Afrika nzima sisi ni wanne kwa madini ya dhaabu, wapili kwa madini ya vito, tunayo madini mengine mengi ambayo hayapatikani mahali pengine isipokuwa Tanzania nayo ni Tanzanite” amesema.
“Haiwezekani tuna utajiri huo alafu watu wetu bado ni masikini ndio maana Rais wetu mnamsikia kila wakati anasema Tanzania sio masikini, unaweza ukasema kuwa wewe ni masikini iwapo hautumii kisawasawa uwezo wako wa kufikiri,” amesema.
Aidha amesema kuwa lengo la serikali la kubadilisha sheria ya madini ni kutaka kuona rasilimali hiyo inawanufaisha Watanzania ili madini yanayopatikana nchini yawe chachu ya kubadilisha maisha ya wananchi
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment