Search This Blog

Tuesday, August 13, 2019

Huyu ndiye mrithi wa Irene Uwoya kwa Dogo Janja


Msanii wa muziki nchini, Dogo Janja amemuweka wazi mpenzi wake mpya baada ya muda mrefu kupita tangu alipoachana na aliyekuwa mke wake, muigizaji IreneUwoya.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, mkali huyo ameweka picha akiwa na mpenzi wake huyo mpya kwenye sikukuu ya Eid El Hajj na kuandika, “kipande hiki EID tunaimaliza kwa style hii.. happy moments with my baby!! Kenya 254 wagwaan”

Hata hivyo hii sio mara ya kwanza kwa Dogo Janja kumuonyesha mpenzi wake huyo Instagram, huwa anam-post mara kwa mara huku akiandika maandishi yanayoashiria wana mahusiano.

Huyu anaweza akawa mrithi wa aliyekuwa mke wake, Irene Uwoya ambaye waliachana mwaka jana baada ya kudumu kwa kipindi kifupi kwenye ndoa.

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...