Search This Blog

Sunday, August 25, 2019

Polisi kumkamata Mgombea Urais Tunisia


Jaji Mkuu wa Fedha wa Tunisia alitoa hati ya kukamwa kwa mgombea wa urais Nabil Karoui kwa madai ya kukwepa kodi na utakatishaji fedha. Pia Waraka wa pili ulitolewa wa kumtia kizuizini kaka wa Nabil Karoui, Ghazi Karoui.

Mmiliki huyo mkubwa wa vyombo vya habari ni mpinzani mkubwa kwenye uchaguzi wa urais unaotarajiwa kufanyika Septemba 15 mwaka huu.

Kituo cha televisheni kinachomilikiwa na Karoui pamoja na vyombo vingine vya habari vilizuiliwa na tume ya uchaguzi na mamlaka ya kusimamia vyombo vya habari kwa madai ya kutokuwa na leseni.

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...