Search This Blog

Saturday, August 17, 2019

Picha: Bonaza la kuadhimisha miaka 8 ya kuanzishwa kwa mamlaka ya viwanja vya ndege Zanzibar


Na Thabit Hamidu, Zanzibar

Taasisi mbalimbali za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar zimeshiriki katika Bonaza la kuadhimisha miaka 8 tangu kuanzishwa kwa mamlaka ya viwanja vya ndege Zanzibar ambapo bonaza hilo limefanyika kisiwani Pemba na kushirikisha taasisi mbali mbali za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Baadhi ya Taasisi hizo za Serikali zilizoshirkia katika Bonaza hilo ni ZECO, Mamalaka ya viwanja vya Ndege, Wizara ya Fedha na Mipango, Bonaza hilo lilishirikisha michezo kwa wanawake na waunaume.


Bonaza hilo lilifunguliwa na Mwenyekiti Mstaafu wa Bodi ya Mmalaka ya viwanja vya ndege Zanzibar Abdullghan Msoma ambapo alizitaka Taasisi za kiserikali zilizoshiriki bonaza hilo kuwa na wamoja na kujenga uhusiano mzuri wa Taasisi zao.

“Lengo la Bonaza hili ni kukuza uhusiano mzuri wa taasisi zilizokuwa chini ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ)” alisema mwenyekiti huyo mstaafu wa Bodi ya Mamlaka hiyo.

Katika Bonaza hilo limeshirikisha michezo mbalimbali kama vile Mpira wa Miguu, kuvuta kamba na michezo mingine huku Timu ya Mpira wa miguu kutoka wizara ya Fedha na mipango ofisi ya Unguja wakifanikiwa kuwa mabingwa  mara baada ya kuingia fainali kuwafunga timu ya wafanyakazi wa uwanja wa ndege Pemba kwa goli moja kwa bila.

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...