
Afisa Mkuu wa Wateja Wadogo na wa Kati Benki ya NMB – Filbert Mponzi akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari wa kutangaza matokeo ya hati fungani ya Benki hiyo katika ofisi za NMB jana jijini Dar es Salaam. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa NMB – Ruth Zaipuna.

Afisa Mkuu wa Fedha, Ruth Zaipuna akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari wa kutangaza matokeo ya hati fungani ya Benki hiyo katika ofisi za NMB jana jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Ofisa Mkuu wateja wadogo na wakati (Chief Retail Banking), Filbert Mponzi na Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Masoko ya Fedha (Head, Global Markets Treasury department), Gladness Deogratius.
***********
BENKI ya NMB, imetangaza matokeo ya mauzo ya toleo la tatu laprogramu ya hati fungani ya benki hiyo, ambako imekusanya Sh. Bilioni83.3 sawa na asilimia 333 ya mauzo yaliyotarajiwa awali ya Sh. Bilioni 25.Mauzo ya toleo la tatu la hati fungani ya NMB yalifunguliwa Juni 10 na kufungwa Julai 8, mwaka huu, ambako kipindi hicho cha miezi miwili,kilikuja baada ya Mamlaka ya Masoko na Mitaji na Dhamana (CMSA),kutoa idhini ya mauzo hayo.
Akizungumza katika hafla ya kutangaza matokeo hayo, iliyofanyika jijiniDar es Salaam jana, Afisa Mkuu wa Fedha , Ruth Zaipuna, alisema waokama benki wanajivunia kiwango hicho cha mauzo, kinachothibitishaimani ya wananchi na jamii kwa benki yake.
Zaipuna alibainisha kuwa, tayari NMB imeyapokea na kuyakubali maombiyote na kwamba waombaji wote wa manunuzi ya hati funganiwametaarifiwa na kwamba leo Agosti 2, wanaorodhesha hati funganizote, kabla ya wanunuzi kukabidhiwa vyeti mwezi mmoja ujao.
Alifafanua ya kwamba, mauzo hayo ya kiwango cha juu kulikowalivyotarajia, yanaiongezea benki nguvu ya kiuchumi katika kufanikishautoaji wa mikopo kwa wateja wao na kwamba mchakato mzimaumeshirikisha zaidi ya matawi 200 kote nchini.
“NMB inatoa shukrani za dhati kwa taasisi zote zilizofanikisha uuzwaji watoleo la tatu la hati fungani ya NMB, ikiwemo CMSA, Soko la Hisa la Dar esSalaam (DSE), Mshauri Kiongozi wa NMB, Stanbic Bank Tanzania Ltd naDalali Mfadhili wa NMB, Orbit Securities Company Ltd,” alisema Zaipuna.
Hati fungani ni aina ya uwekezaji, ambao unamuwezesha mteja kuwekezapesa katika taasisi (hasa shirika la kibiashara au Serikali), kwa kuikopeshafedha kwa muda maalum na kwa riba isiyobadilika. Riba ya hati funganiza NMB kwa mwaka ni asilimia 10.
Mteja anaponunua Hati Fungani ya NMB, anakuwa ameikopesha benkifedha zake, ambako NMB inaahidi kurejesha fedha zake (msingi) katika kipindi maalum cha ukomavu. Kuanzia muda uliowekeza hadi muda waukomavu ambao unakuwa miaka mitatu.
No comments:
Post a Comment