*BASATA yaibariki bodi mpya na kuwataka kufanya kazi kwa kuzingatia maadili, sheria, kanuni na taratibu
Na Leandra Gabriel, Michuzi TV
BODI maalumu itakayosimamia mashindano ya urembo, utalii na utamaduni maarufu kama Miss Toursim Tanzania imezinduliwa rasmi jana jijini Dar es Salaam na hiyo ni kufuatia kushindwa kwa usimamizi wa mashindano hayo kupitia taasisi iliyokuwa inasimamia mashindano hayo hali iliyopelekea kurekebishwa kwa mfumo wa mashindano hayo kwa kuimarisha usimamizi wa mashindano pamoja na kupunguza gharama za uendeshaji.
Akizungumza mara baada ya kuizindua bodi hiyo Kaimu Katibu Mtendaji Mkuu wa baraza la sanaa la taifa (BASATA) Vivian Shalua amepongeza uamuzi wa kuanzishwa kwa bodi maalumu itakayosimamia mashindano hayo tofauti na ilivyokuwa awali huku akiwataka wajumbe wa bodi hiyo kufanya kazi kwa kuzingatia maadili, sheria, kanuni na taratibu na kuipepereshusha vyema bendera ya Tanzania.
Shalua amesema kuwa mwaka 2013 baraza hilo ilitoa muda wa wasimamizi wa mashindano hayo kujichunguza na kuboresha mashindano na wanaamini bodi hiyo itafanyavizuri zaidi kwa kuwa wamekuwa wakishirikisha baraza la sanaa kwa kila hatua na katika vikao vyao wamedhamiria kutangaza vivutio vya nchi kitaifa na kimataifa na kuwaomba wadhamini kujitokeza ili kuweza kudhamini mashindano hayo.
Kwa upande wake Rais na mwenyekiti wa bodi hiyo Gideon Chipungahelo amesema kwamba baada ya kutathimini na kupanga mikakati kuhusiana na mashindano hayo wamekuja na nguvu mpya kwa kuandaa shindano la kitaifa la miss utalii Tanzania kwa kuhusisha zaidi ya nchi 100 duniani pamoja na washiriki watakaowakilisha Tanzania kupitia kanda maalumu za ushiriki.
Chipungahelo amesema kuwa bodi inayosimamia mashindano hayo ipo imara na yataendeshwa kwa kufuata kanuni, sheria na taratibu kwa malengo ya kulitangaza taifa kupitia utalii, utamaduni pamoja na mila za kitanzania.
Vilevile amewashauri wasanii na wadau wa Sanaa kuwatumia wataalamu kutoka BASATA ili waweze kufahamu namna bora za uendeshaji wa shughuli za sanaa kote nchini.
Mchakato wa mashindano hayo ya urembo unatarajiwa kuanza mwishoni mwa mwezi Agosti na utahusisha kanda nane katika Mikoa yote nchini na kubeba kauli mbiu ya, "Miss Utalii Tanzania ni Alama ya Urithi wa Taifa- Utalii mi Maisha, Utamaduni ni Uhai wa Taifa-"
Rais na mwenyekiti wa bodi ya Shindano la Miss Utalii ( Miss Toursim Tanzania) ,Gideon Chipungahelo (kulia) akimshukuru Kaimu Katibu Mtendaji Mkuu wa Baraza la sanaa la Taifa (BASATA) ,Vivian Shalua mara baada ya kumaliza kikao chao na kupatikana kwa bodi mpya ya shindano hilo na kuitangaza rasmi mbele ya Waandishi wa Habari,jana jijini Dar.Picha na Michuzi Jr-Michuzi Media

Rais na mwenyekiti wa bodi ya Shindano la Miss Utalii ( Miss Toursim Tanzania) ,Gideon Chipungahelo (kulia) akizungumza mbele ya Waandishi wa habari mikakati mipya ya shindano hilo,mara baada ya kutangazwa bodi mpya ya shindano hilo,huku wakishirikiana bega kwa bega na Baraza la sanaa la Taifa (BASATA)

Kaimu Katibu Mtendaji Mkuu wa Baraza la sanaa la Taifa (BASATA) ,Vivian Shalua akizungumza mbele ya Waandishi wa Habari (hawapo pichani),mara baada ya kuizindua bodi mpya ya Miss Tourism Tanzania,ambapo pia alipongeza uamuzi wa kuanzishwa kwa bodi maalumu itakayosimamia mashindano hayo tofauti na ilivyokuwa awali huku akiwataka wajumbe wa bodi hiyo kufanya kazi kwa kuzingatia maadili, sheria, kanuni na taratibu na kuipepereshusha vyema bendera ya Tanzania.
Bodi mpya ya Miss Tourism Tanzania ikiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa BASATA katika meza kuu,wakati wa Mkutano na Waandishi wa Habari.

Rais na mwenyekiti wa bodi ya Shindano la Miss Utalii ( Miss Toursim Tanzania) ,Gideon Chipungahelo akiwaonesha wanahabari (hawapo pichani) muonekano mpya wa shindano hilo mara baada ya kuzinduliwa upya na Kaimu Katibu Mtendaji Mkuu wa Baraza la sanaa la Taifa (BASATA) ,Vivian Shalua

Rais na mwenyekiti wa bodi ya Shindano la Miss Utalii ( Miss Toursim Tanzania) ,Gideon Chipungahelo akiwashukuru wanahabari (hawapo pichani) na Wadau mbalimbali waliojitokeza kushuhudia tukio hilo adhimu,kushoto ni Kaimu Katibu Mtendaji Mkuu wa Baraza la sanaa la Taifa (BASATA) ,Vivian Shalua

Bodi mpya ya Miss Tourism Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa BASATA

No comments:
Post a Comment