Search This Blog

Friday, August 23, 2019

NEC yamteua Anna Kajigili kuwa Diwani Viti Maalum Chadema


Kwa mujibu wa Kifungu cha 86A (8) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Tume ya Taifa ya Uchaguzi katika kikao chake cha tarehe 23 Agosti, 2019 imemteua Ndg. Anna Alinanine Kajigili kuwa Diwani wa Wanawake wa Viti Maalum katika Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.

Uteuzi huu umefanyika baada ya kupokea taarifa kutoka kwa Waziri mwenye dhamana ya Serikali za Mitaa, ambaye kwa kuzingatia masharti ya kifungu cha 13(1) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, alitaarifu Tume ya Taifa ya Uchaguzi uwepo wa nafasi hiyo wazi ya Diwani wa wanawake wa Viti Maalum, kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) baada ya aliyeteuliwa awali kujiuzulu uanachama wa CHADEMA.

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...