Search This Blog
Wednesday, August 14, 2019
Ndoa ya Rooney Mashakani Kisa Pombe, Mkewe Atimka Marekani Kuepuka Aibu
Aliyekuwa mchezaji wa Manchester United, Wayne Rooney amelazimika kuacha kabisa kunywa pombe ili kuokoa ndoa yake na mkewe Coleen ambaye amezaa nae watoto wa nne.
The Sun imeripoti kuwa Rooney amekuwa akiishi Marekani na familia yake tangu mwaka uliopita, lakini tayari mkewe ameondoka huko na kurudi Uingereza kutokana na vituko vya ulevi vinavyoendelea.
Wakati uhusiano wake na mkewe umekuwa wa mashaka kutokana na matukio mbali mbali ya ulevi wa Rooney. Mapema mwaka huu alikamatwa na polisi kwa kulewa kupita kiasi akiwa uwanja wa ndege Marekani.
Kwa mujibu wa jarida la Mirror, Rooney anatarajiwa kurudi Uingereza mwezi Oktoba na yupo tayari kujiunga na Derby ya nchini humo ili kutumia fursa ya kuwa karibu na mkewe ambapo pia atakutana na mtu wa ushauri nasaha ili kurejesha amani katika ndoa yake.
Inasemekana maamuzi ya Rooney kurudi Uingereza yatamgharimu mamilioni ya pesa. Lakini mkewe alitaka Rooney ampe kipaumbele yeye Coleen na watoto.
Hivyo Rooney ameamua kufanyia kazi hilo “si tatizo kupoteza pesa kwani ni thamani zaidi kumfanya Coleen awe na furaha”
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment