Search This Blog
Thursday, August 15, 2019
Lijue Gari ghali zaidi duniani, Cristiano Ronaldo atajwa kulinunua
Hili gari, Bugatti La Voiture Noire ndilo gari ghali zaidi katika historia ya dunia, likiwa linagharimu US Dollar Milioni 18.7 sawa na Tsh. Bilioni 43.1.
Gari hili lilizinduliwa Machi 5 mwaka huu kwenye maonyesho ya magari ya kimataifa, Geneva International Motor Show kuadhimisha miaka 100 tangu kuanzishwa kwa kampuni ya Bugatti.
Wakati wa uzinduzi wake, gari hili tayari lilikuwa limelipiwa na mnunuzi ambaye hakutaka kujulikana. Bwana huyo alilipia gari hilo hata kabla kutengenezwa kwenye kiwanda.
Kuna fununu ambazo zingali hazijathibitishwa kwamba gari hilo lilinunuliwa na nyota wa soka Cristiano Ronaldo.
Gari hili ambalo lina injini yenye ukubwa wa 8,000cc na turbo nne, linabeba abiria wawili na linaweza kuenda kasi ya kilomita 465 kwa saa. Kampuni ya Bugatti ilitengeneza toleo moja pekee ya La Voiture Noire. Hivyo basi hakuna mwingine atakayekuwa na gari sawa isipokuwa aliyenunua hili toleo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...



No comments:
Post a Comment