Search This Blog
Thursday, August 15, 2019
Dodoma FC yaibana Mbeya City
Na Ezekiel Mtonyole, Dodoma
Timu ya Dodoma FC imefanikiwa kutoka sare ya kutokufungana na timu ya Mbeya city inayoshiriki ligi kuu kutoka Jijini Mbeya, katika mchezo wa kujipima nguvu kwa timu hizo kuelekea mashindano mbalimbali kwa timu hizo, mchezo uliofanyika katika uwanja wa jamhuri Dodoma.
Timu ya Dodoma fc ambayo inayoshiriki ligi daraja la kwanza, na kwa sasa ikiwa inamilikiwa na halmashauri ya Jiji la Dodoma, licha ya kucheza na timu ngumu ya ligi kuu ilionekana kucheza vizuri kiasi cha kuwaridhisha mashabiki waliokuwapo kushuhudia mchezo huo.
Mara baada ya mchezo huo kocha wa Mbeya city Juma Mwambusi amesifu uwezo mkubwa uliooneshwa na Dodoma fc na kusema kuwa kupitia mchezo huo ameona mapungufu yaliyopo katika timu yake
“Kweli tumepata upinzani mkubwa kutoka kwa Dodoma FC na mbinu ambazo niliwapa wachezaji wangu hazikuweza kufanikiwa kwa sababu timu ya Dodoma fc walikuwa wazuri katika kukaba nafasi ni kipimo kizuri kwetu” amesema Mwambusi.
Kwa upande wake Kocha wa Dodoma FC, Mbwana Makata amesema wachezaji wake walijitahidi kufuata aelekezo yake, na amesema amepanga kutumia timu za ligi kuu ili kuendelea kuimarisha timu yake tayari kwa mapambano ya ligi daraja la kwanza.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment